59 Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakaria.
60 Lakini mama yake akasema, “Sivyo, bali ataitwa Yohane.”
61 Wakamwambia, “Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina hilo?”
62 Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake apewe jina gani.
63 Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: “Yohane ndilo jina lake.” Wote wakastaajabu.
64 Papo hapo, midomo na ulimi wake Zakaria vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu.
65 Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.