70 Aliahidi hapo kalekwa njia ya manabii wake watakatifu,
71 kwamba atatuokoa mikononi mwa maadui zetuna kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72 Alisema atawahurumia wazee wetu,na kukumbuka agano lake takatifu.
73 Alimwapia Abrahamu babu yetu,kwamba atatujalia sisi
74 tukombolewe mikononi mwa maadui zetu,tupate kumtumikia bila hofu,
75 tuwe wanyofu na waadilifu mbele yake,siku zote za maisha yetu.
76 Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu,utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;