75 tuwe wanyofu na waadilifu mbele yake,siku zote za maisha yetu.
76 Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu,utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;
77 kuwatangazia watu kwamba wataokolewakwa kuondolewa dhambi zao.
78 Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma.Atatuchomozea mwanga kutoka juu,
79 na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo,aongoze hatua zetu katika njia ya amani.”
80 Mtoto akakua, akapata nguvu rohoni. Alikaa jangwani mpaka alipojionesha rasmi kwa watu wa Israeli.