3 Utupe daima chakula chetu cha kila siku.
4 Utusamehe dhambi zetu,maana sisi tunawasamehe wote waliotukosea;wala usitutie katika majaribu.’”
5 Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu anaye rafiki, akaenda kwake usiku wa manane, akamwambia: ‘Rafiki, tafadhali niazime mikate mitatu,
6 kwa kuwa rafiki yangu amepitia kwangu akiwa safarini nami sina cha kumpa.’
7 Naye, akiwa ndani angemjibu: ‘Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!’
8 Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake, lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote anachohitaji.
9 Kwa hiyo, ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni mlango nanyi mtafunguliwa.