5 Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu anaye rafiki, akaenda kwake usiku wa manane, akamwambia: ‘Rafiki, tafadhali niazime mikate mitatu,
6 kwa kuwa rafiki yangu amepitia kwangu akiwa safarini nami sina cha kumpa.’
7 Naye, akiwa ndani angemjibu: ‘Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!’
8 Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake, lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote anachohitaji.
9 Kwa hiyo, ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni mlango nanyi mtafunguliwa.
10 Maana yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata na abishaye mlango hufunguliwa.
11 Mtoto akimwomba baba yake samaki, je, atampa nyoka badala ya samaki?