56 Enyi wanafiki! Mnajua kutabiri hali ya hewa kwa kuangalia hali ya nchi na anga; kwa nini, basi, hamwezi kujua maana ya nyakati hizi?
57 “Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya?
58 Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.
59 Hakika hutatoka huko, nakuambia, mpaka utakapomaliza kulipa senti ya mwisho.”