15 Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa, alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa.
16 Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.
17 Hapo Yesu akasema, “Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi?
18 Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?”
19 Halafu akamwambia huyo mtu, “Simama, uende zako; imani yako imekuponya.”
20 Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, “Ufalme wa Mungu utakuja lini?” Naye akawajibu, “Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana.
21 Wala hakuna atakayeweza kusema, ‘Uko hapa’, au ‘Uko pale’. Kwa kweli ufalme wa Mungu uko kati yenu.”