38 Naye akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”
39 Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini yeye akazidi kupaza sauti: “Mwana wa Daudi, nihurumie!”
40 Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu alipofika karibu, Yesu akamwuliza,
41 “Unataka nikufanyie nini?” Naye akamjibu, “Bwana, naomba nipate kuona.”
42 Yesu akamwambia, “Ona! Imani yako imekuponya.”
43 Na mara huyo kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.