11 Mwambieni mwenye nyumba: ‘Mwalimu anakuuliza, kiko wapi kile chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?’
12 Naye atawaonesheni chumba kikubwa ghorofani ambacho kimepambwa. Andalieni humo.”
13 Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia; wakaandaa karamu ya Pasaka.
14 Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakula pamoja na mitume wake.
15 Akawaambia, “Nimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu.
16 Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika ufalme wa Mungu.”
17 Kisha akatwaa kikombe cha divai, akashukuru, akasema, “Pokeeni, mgawane.