31 Mara macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua; lakini yeye akatoweka kati yao.
32 Basi, wakaambiana, “Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?”
33 Wakaondoka saa ileile, wakarudi Yerusalemu; wakawakuta wale mitume kumi na mmoja na wale wengine waliokuwa pamoja nao wamekusanyika
34 wakisema, “Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simoni.”
35 Basi, hao wafuasi wawili wakawajulisha yale yaliyowapata njiani, na jinsi walivyomtambua katika kumega mkate.
36 Walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akawaambia “Amani iwe nanyi.”
37 Wakashtuka na kushikwa na hofu wakidhani wameona mzimu.