40 Baada ya kusema hayo, akawaonesha mikono na miguu.
41 Wakiwa bado katika hali ya kutosadiki kwa sababu ya furaha yao, na wakiwa wanastaajabu, akawauliza, “Mnacho chakula chochote hapa?”
42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.
43 Akakichukua, akala, wote wakimwona.
44 Halafu akawaambia, “Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi: Kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika sheria ya Mose na katika vitabu vya manabii na katika kitabu cha Zaburi.”
45 Kisha, akaziangazia akili zao ili wapate kuelewa Maandiko Matakatifu.
46 Akawaambia, “Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu,