50 Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki.
51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni.
52 Wao wakamwabudu, kisha wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kubwa:
53 Wakakaa muda wote hekaluni wakimsifu Mungu.