9 Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa hekalu, akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini
10 kwa maana imeandikwa:‘Atawaamuru malaika wake wakulinde,’
11 na tena,‘Watakuchukua mikononi mwao,usije ukajikwaa mguu kwenye jiwe.’”
12 Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”
13 Ibilisi alipokwisha mjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.
14 Hapo Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.
15 Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote.