4 Wanafunzi wake wakamwuliza, “Hapa nyikani itapatikana wapi mikate ya kuwashibisha watu hawa wote?”
5 Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakamjibu, “Saba.”
6 Basi, akawaamuru watu wakae chini. Akaitwaa ile mikate saba, akamshukuru Mungu, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu, nao wakawagawia.
7 Walikuwa pia na visamaki vichache. Yesu akavibariki, akaamuru vigawiwe watu vilevile.
8 Watu wakala, wakashiba. Wakakusanya makombo wakajaza vikapu saba.
9 Nao waliokula walikuwa watu wapatao 4,000. Yesu akawaaga,
10 na mara akapanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda wilaya ya Dalmanutha.