12 Lakini, mtu ana thamani kuliko kondoo! Basi, ni halali kutenda mema siku ya Sabato.”
13 Kisha akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako.” Akaunyosha, nao ukawa mzima kabisa kama ule mwingine.
14 Basi, Mafarisayo wakatoka nje, wakashauriana jinsi watakavyomwangamiza Yesu.
15 Lakini Yesu alipojua jambo hilo, akatoka mahali pale. Watu wengi walimfuata, akawaponya wagonjwa wote,
16 akawaamuru wasiwaambie watu habari zake,
17 ili yale aliyosema Mungu kwa njia ya nabii Isaya yatimie:
18 “Tazama mtumishi wangu niliyemteua,mpendwa wangu anipendezaye moyoni.Nitaiweka roho yangu juu yake,naye atatangaza hukumu yangu kwa mataifa yote.