17 ili yale aliyosema Mungu kwa njia ya nabii Isaya yatimie:
18 “Tazama mtumishi wangu niliyemteua,mpendwa wangu anipendezaye moyoni.Nitaiweka roho yangu juu yake,naye atatangaza hukumu yangu kwa mataifa yote.
19 Hatakuwa na ubishi wala kupiga kelele,wala sauti yake haitasikika barabarani.
20 Mwanzi uliopondeka hatauvunja,wala utambi ufukao moshi hatauzima,mpaka atakapoifanya hukumu ya haki itawale.
21 Kwake yeye mataifa yatakuwa na matumaini.”
22 Hapo watu wakamletea Yesu mtu mmoja kipofu na ambaye alikuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo. Yesu akamponya hata akaweza kusema na kuona.
23 Umati wote wa watu ulishangaa ukasema, “Je, huenda ikawa huyu ndiye Mwana wa Daudi?”