12 Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
13 Ndio maana ninasema nao kwa mifano, kwa sababu wanatazama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawaelewi.
14 Kwao yametimia yale aliyosema nabii Isaya:‘Kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa.Kutazama mtatazama, lakini hamtaona.
15 Maana akili za watu hawa zimepumbaa,wameyaziba masikio yao,wameyafumba macho yao.La sivyo, wangeona kwa macho yao,wangesikia kwa masikio yao,wangeelewa kwa akili zao,na kunigeukia, asema Bwana,nami ningewaponya.’
16 “Lakini heri yenu nyinyi, maana macho yenu yanaona na masikio yenu yanasikia.
17 Kweli nawaambieni, manabii na watu wengi wema walitamani kuyaona yale mnayoyaona, wasiyaone, na kuyasikia yale mnayoyasikia, wasiyasikie.
18 “Basi, nyinyi sikilizeni maana ya mfano huo wa mpanzi.