43 Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
44 Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.”
45 Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake?
46 Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakapokuja atamkuta akifanya hivyo.
47 Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote.
48 Lakini kama mtumishi mbaya akijisemea moyoni: ‘Bwana wangu amekawia kurudi,’
49 kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula na kunywa pamoja na walevi,