3 Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.
4 Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao.
5 Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wasichana wote walisinzia, wakalala.
6 Usiku wa manane kukawa na kelele: ‘Haya, haya! Bwana arusi anakuja; nendeni kumlaki.’
7 Hapo wale wasichana wote wakaamka, wakazitayarisha taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara: ‘Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.’
9 Lakini wale wenye busara wakawaambia, ‘Hayatatutosha sisi na nyinyi! Afadhali mwende dukani mkajinunulie wenyewe!’