6 Usiku wa manane kukawa na kelele: ‘Haya, haya! Bwana arusi anakuja; nendeni kumlaki.’
7 Hapo wale wasichana wote wakaamka, wakazitayarisha taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara: ‘Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.’
9 Lakini wale wenye busara wakawaambia, ‘Hayatatutosha sisi na nyinyi! Afadhali mwende dukani mkajinunulie wenyewe!’
10 Basi, wale wasichana wapumbavu walipokwenda kununua mafuta, bwana arusi akafika, na wale wasichana waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye katika jumba la harusi, kisha mlango ukafungwa.
11 Baadaye wale wasichana wengine wakaja, wakaita: ‘Bwana, Bwana, tufungulie!’
12 Lakini yeye akawajibu, ‘Nawaambieni kweli, siwajui nyinyi.’”