29 Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, “Shikamoo mfalme wa Wayahudi!”
30 Wakamtemea mate, wakauchukua ule mwanzi, wakampiga nao kichwani.
31 Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
32 Walipokuwa wakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lake Simoni, mwenyeji wa Kurene, wakamlazimisha kuuchukua msalaba wake Yesu.
33 Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, mahali pa Fuvu la Kichwa,
34 wakampa mchanganyiko wa divai na kitu kichungu. Lakini Yesu alipoonja akakataa kunywa.
35 Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.