33 Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, mahali pa Fuvu la Kichwa,
34 wakampa mchanganyiko wa divai na kitu kichungu. Lakini Yesu alipoonja akakataa kunywa.
35 Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
36 Wakaketi, wakawa wanamchunga.
37 Juu ya kichwa chake wakaweka shtaka dhidi yake lililoandikwa, “Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi.”
38 Wanyanganyi wawili walisulubiwa pia pamoja naye, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.
39 Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema,