8 Ndio maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu.
9 Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: “Walichukua vipande thelathini vya fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walimtia bei,
10 wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.”
11 Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, “Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamwambia, “Wewe umesema.”
12 Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno.
13 Hivyo Pilato akamwuliza, “Je, husikii mashtaka hayo yote wanayotoa juu yako?”
14 Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata huyo mkuu wa mkoa akashangaa sana.