1 Siku zile Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea:
2 “Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”
3 Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema:“Sauti ya mtu anaita jangwani:‘Mtayarishieni Bwana njia yake,nyosheni barabara zake.’”
4 Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
5 Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka pande zote za Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea,