10 Kwa kuwa Yesu Kristo alitimiza matakwa ya Mungu, sisi tunatakaswa dhambi zetu kwa ile tambiko ya mwili wake aliyotoa mara moja tu, ikatosha.
11 Kila kuhani Myahudi hutoa huduma yake ya ibada ya kila siku na kutoa tambiko zilezile mara nyingi, tambiko ambazo haziwezi kuondoa dhambi.
12 Lakini Kristo alitoa tambiko moja kwa ajili ya dhambi, tambiko ifaayo milele, kisha, akaketi upande wa kulia wa Mungu,
13 anangoja maadui zake wafanywe kama kibao chini ya miguu yake.
14 Basi, kwa tambiko yake moja, amewafanya kuwa wakamilifu milele wote wale wanaotakaswa dhambi zao.
15 Naye Roho Mtakatifu anatupa ushahidi wake. Kwanza anasema:
16 “Hili ndilo agano nitakalofanya nao, siku zijazo, asema Bwana:Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao,na kuziandika akilini mwao.”