10 Hapo mtaweza kuishi kama anavyotaka Bwana na kutenda daima yanayompendeza. Maisha yenu yatakuwa yenye matunda ya kila namna ya matendo mema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu.
11 Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili muweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu.
12 Na kwa furaha mshukuruni Baba, aliyewawezesha nyinyi kuwa na sehemu yenu katika mambo yale aliyowawekea watu wake katika ufalme wa mwanga.
13 Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika ufalme wa Mwanae mpenzi.
14 Kwake yeye tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa.
15 Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana;ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
16 Maana kwake vitu vyote viliumbwakila kitu duniani na mbinguni,vitu vinavyoonekana na visivyoonekana:Wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu.Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake.