1 Basi, ikiwa mmefufuka pamoja na Kristo, panieni mambo ya juu, kule Kristo aliko, ameketi upande wa kulia wa Mungu.
2 Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani.
3 Maana nyinyi mmekufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
4 Uhai wenu halisi ni Kristo, na wakati atakapotokea ndipo nanyi pia mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.
5 Basi, ueni chochote kilicho ndani yenu ambacho ni cha kidunia: Uasherati, uchafu, shauku, tamaa mbaya na uchu (ambao ni sawa na kuabudu sanamu).
6 Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wote wanaomwasi.
7 Wakati mmoja nyinyi pia mliishi kufuatana na mambo hayo, mlipotawaliwa nayo.