3 “Bwana, wamewaua manabii wako na kubomoa madhabahu yako. Ni mimi tu peke yangu niliyebaki, nao wanataka kuniua!”
4 Je, Mungu alimjibu nini? Alimwambia: “Nimejiwekea watu 7,000 ambao hawakumwabudu Baali.”
5 Basi, ndivyo ilivyo pia wakati huu wa sasa: Ipo idadi ya waliobaki ambao Mungu aliwateua kwa sababu ya neema yake.
6 Uteuzi wake unatokana na neema yake, na si kwa sababu ya matendo yao. Maana, kama uteuzi wake ungetegemea matendo ya watu, neema yake haingekuwa neema tena.
7 Sasa, je? Watu wa Israeli hawakukipata kile walichokuwa wanakitafuta; lakini wote walioteuliwa walikipata. Wengine walipumbazwa,
8 kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Mungu ameifanya mioyo yao kuwa mizito,na mpaka leo hii hawawezi kuona kwa macho yaowala kusikia kwa masikio yao.”
9 Naye Daudi anasema:“Karamu zao na ziwe mtego wa kuwanasa,waanguke na kuadhibiwa.