32 Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi wao ili apate kuwahurumia wote.
33 Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichunguziki, na njia zake hazieleweki! Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:
34 “Nani aliyepata kuyajua mawazo ya Bwana?Nani awezaye kuwa mshauri wake?
35 Au, nani aliyempa yeye kitu kwanzahata aweze kulipwa tena kitu hicho?”
36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, vyote vipo kwa uwezo wake na kwa ajili yake. Utukufu na uwe kwake hata milele! Amina.