10 Tena Maandiko yasema:“Furahini, enyi watu wa mataifa;furahini pamoja na watu wake.”
11 Na tena:“Enyi mataifa yote, msifuni Bwana;enyi watu wote, msifuni.”
12 Tena Isaya asema:“Atatokea chipukizi katika ukoo wa Yese,naye atawatawala watu wa mataifa;nao watamtumainia.”
13 Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.
14 Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba nyinyi pia mmejaa wema, elimu yote, na mnaweza kushauriana nyinyi kwa nyinyi.
15 Lakini nimewaandikia hapa na pale katika barua hii bila woga, nipate kuwakumbusheni juu ya mambo fulani. Nimefanya hivyo kwa sababu ya neema aliyonijalia Mungu
16 ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa. Ni jukumu langu la kikuhani kuihubiri Habari Njema ya Mungu ili watu wa mataifa mengine wapate kuwa tambiko inayokubaliwa na Mungu, tambiko iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.