6 ili nyinyi nyote, kwa nia moja na sauti moja, mumtukuze Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
7 Basi, karibishaneni kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama naye Kristo alivyowakaribisheni.
8 Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;
9 ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Kwa hiyo nitakusifu miongoni mwa watu wa mataifa.Nitaziimba sifa za jina lako.”
10 Tena Maandiko yasema:“Furahini, enyi watu wa mataifa;furahini pamoja na watu wake.”
11 Na tena:“Enyi mataifa yote, msifuni Bwana;enyi watu wote, msifuni.”
12 Tena Isaya asema:“Atatokea chipukizi katika ukoo wa Yese,naye atawatawala watu wa mataifa;nao watamtumainia.”