6 Lakini nyinyi mnawadharau watu maskini! Je, matajiri si ndio wanaowakandamiza na kuwapeleka mahakamani?
7 Je, si haohao wanaolitukana hilo jina lenu zuri mlilopewa?
8 Kama mnaitimiza ile sheria ya ufalme kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe”, mtakuwa mnafanya vema kabisa.
9 Lakini mkiwabagua watu, basi, mwatenda dhambi, nayo sheria inawahukumu nyinyi kuwa mna hatia.
10 Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja sheria yote.
11 Maana yuleyule aliyesema: “Usizini,” alisema pia “Usiue.” Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini, lakini umeua, wewe umeivunja sheria.
12 Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru.