1 Hapo mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu.
2 Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu.
3 Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye.
4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.
5 Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda.
6 Mungu alimtuma mtu mmoja jina lake Yohane,
7 ambaye alikuja kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wake watu wote wapate kuamini.