16 Thoma (aitwaye Pacha) akawaambia wanafunzi wenzake, “Twendeni nasi tukafe pamoja naye!”
17 Yesu alipofika huko alikuta Lazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne.
18 Kijiji cha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemu, umbali upatao kilomita tatu.
19 Wayahudi wengi walikuwa wamefika kwa Martha na Maria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao.
20 Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani.
21 Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!
22 Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.”