1 “Mimi ni mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda yeye huliondoa, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi.
3 Nyinyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya ule ujumbe niliowaambieni.
4 Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi haliwezi peke yake kuzaa matunda lisipobaki katika mzabibu, hali kadhalika nanyi hamwezi kuzaa matunda msipokaa ndani yangu.