28 Huyo mama akauacha mtungi wake pale, akaenda mjini na kuwaambia watu,
29 “Njoni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote niliyotenda! Je, yawezekana kuwa yeye ndiye Kristo?”
30 Watu wakatoka mjini, wakamwendea Yesu.
31 Wakati huohuo wanafunzi wake walikuwa wanamsihi Yesu: “Mwalimu, kula chakula.”
32 Lakini Yesu akawaambia, “Mimi ninacho chakula msichokijua nyinyi.”
33 Wanafunzi wake wakaulizana, “Je, kuna mtu aliyemletea chakula?”
34 Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.