48 Je, mmekwisha kumwona hata mmoja wa viongozi wa watu, au mmoja wa Mafarisayo aliyemwamini?
49 Lakini umati huu haujui sheria ya Mose; umelaaniwa!”
50 Mmoja wao alikuwa Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu. Basi, yeye akawaambia,
51 “Je, sheria yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza na kujua anafanya nini?”
52 Nao wakamjibu, “Je, wewe pia umetoka Galilaya? Haya, kayachunguze Maandiko Matakatifu nawe utaona kwamba Galilaya hakutoki kamwe nabii!”[
53 Basi, wote wakaondoka, kila mtu akaenda nyumbani;