32 Tangu mwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
33 Kama mtu huyu hakutoka kwa Mungu, hangeweza kufanya chochote!”
34 Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi, wakamfukuza sunagogini.
35 Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuza sunagogini. Basi, alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”
36 Huyo mtu akajibu, “Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ili nipate kumwamini.”
37 Yesu akamwambia, “Umekwisha mwona, naye ndiye anayesema nawe sasa.”
38 Basi, huyo mtu akasema, “Ninaamini Bwana!” Akamsujudia.