34 Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi, wakamfukuza sunagogini.
35 Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuza sunagogini. Basi, alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”
36 Huyo mtu akajibu, “Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ili nipate kumwamini.”
37 Yesu akamwambia, “Umekwisha mwona, naye ndiye anayesema nawe sasa.”
38 Basi, huyo mtu akasema, “Ninaamini Bwana!” Akamsujudia.
39 Yesu akasema, “Mimi nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu, kusudi wasioona wapate kuona, na wale wanaoona wawe vipofu.”
40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja naye walisikia maneno hayo, wakamwuliza, “Je, sisi pia ni vipofu?”