18 Daudi alisema watu wa Yuda wafundishwe ombolezo hilo, nalo limeandikwa katika kitabu cha Yashari. Daudi aliimba,
19 “Walio fahari yako, ee Israeli,wameuawa milimani pako.Jinsi gani mashujaa walivyoanguka!
20 Jambo hilo msiuambie mji wa Gathiwala katika mitaa ya Ashkeloni.La sivyo, wanawake Wafilisti watashangilia,binti za wasiotahiriwa, watafurahi.
21 “Enyi milima ya Gilboa,msiwe na umande au mvua juu yenu.Wala mashamba yenu daima yasitoe chochote.Maana huko ngao za shujaa zilitiwa najisi,ngao ya Shauli haikupakwa mafuta.
22 “Upinde wa Yonathani kamwe haukurudi nyuma,upanga wa Shauli kamwe haukurudi bure,daima ziliua wengi.Naam, ziliua mashujaa.
23 “Shauli na Yonathani,watu wa ajabu na wakupendeza.Maishani na kifoni hawakutengana.Walikuwa wepesi kuliko tai,naam, wenye nguvu kuliko simba.
24 “Wanawake wa Israeli, mlilieni Shauli!Aliwavika mavazi mekundu ya fahari,aliyatarizi mavazi yenu kwa dhahabu.