19 Walinivamia nilipokuwa taabuni,lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu.
20 Alinileta, akaniweka mahali pa usalama,alinisalimisha, kwani alipendezwa nami.
21 “Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu;alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia.
22 Maana, nimefuata njia za Mwenyezi-Mungu,wala sikujitenga na Mungu wangu kwa uovu.
23 Nimeshika maagizo yake yote,sikuacha kufuata masharti yake.
24 Mbele yake sikuwa na hatia,nimejikinga nisiwe na hatia.
25 Mwenyezi-Mungu amenituza kadiri ya uadilifu wangu,yeye anajua usafi wangu.