46 Wageni walikufa moyo;wakaja kutoka ngome zao wakitetemeka.
47 “Mwenyezi-Mungu yu hai!Asifiwe mwamba wangu!Atukuzwe Mungu wangu, mwamba wa wokovu wangu.
48 Yeye ameniwezesha kulipiza kisasina kuyatiisha mataifa chini yangu.
49 Ameniokoa kutoka adui zangu.Ee Mwenyezi-Mungu, ulinikuza juu ya wapinzani wanguna kunisalimisha mbali na watu wakatili.
50 “Kwa hiyo, nitakutukuza kati ya mataifa,ee Mwenyezi-Mungu, nitaliimbia sifa jina lako.
51 Mungu humjalia mfalme wake ushindi mkubwa;humwonesha fadhili zake huyo aliyemweka wakfu,naam, humfadhili Daudi na wazawa wake milele.”