2 Ni lazima mniheshimu mimi kwa matendo yenu, msiponisikiliza nitawaleteeni laana, vitu vyote mnavyopewa kwa mahitaji yenu nitavilaani. Na kweli nimekwisha kuvilaani, kwa sababu hamuyatilii maanani maagizo yangu.
3 Tazama, nitawaadhibu watoto wenu na nyinyi wenyewe kutokana na uovu wenu, na kuzipaka nyuso zenu mavi ya wanyama wenu wa tambiko. Nitawafukuza mbali nami.
4 Hivyo mtajua kuwa nimewapeni amri hii ili agano langu na ukoo wa Lawi liwe la kudumu.
5 “Katika agano hilo, niliwaahidi uhai na amani na kwamba wao ni lazima kunicha mimi, nao kwa upande wao walinicha mimi, wakaliogopa jina langu.
6 Mafundisho yao yalikuwa ya kweli na kamwe hawakufundisha uongo. Mimi na wao tulikaa kwa amani. Si kwamba walitenda haki tu, bali waliwafundisha wengine kutotenda maovu.
7 Ni wajibu wa makuhani kuwafundisha watu maarifa ya kweli juu ya Mungu. Watu wawaendee kujifunza matakwa yangu kwao, kwani makuhani ni wajumbe wa Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
8 “Bali nyinyi makuhani mmegeuka mkaiacha njia ya haki. Mafundisho yenu yamewaongoza watu wengi katika kutenda mabaya. Mmelivunja agano nililofanya nanyi.