1 Mimi ni mtu niliyepata matesokwa fimbo ya ghadhabu yake Mungu.
2 Amenichukua akanipelekampaka gizani kusiko na mwanga.
3 Amenyosha mkono wake dhidi yangu mimi tu,akanichapa tena na tena mchana kutwa.
4 Amenichakaza ngozi na nyama,mifupa yangu ameivunja.
5 Amenizingira na kunizungushiauchungu na mateso.
6 Amenikalisha gizanikama watu waliokufa zamani.
7 Amenizungushia ukuta nisitoroke,amenifunga kwa minyororo mizito.