Maombolezo 4 BHN

Yerusalemu baada ya kuangamia

1 Jinsi gani dhahabu yetu ilivyochujuka,dhahabu safi kabisa ilivyobadilika!Mawe ya thamani yametawanywayamesambaa barabarani kote.

2 Watoto wa Siyoni waliosifika sana,waliothaminiwa kama dhahabu safi,jinsi gani sasa wamekuwa kama vyombo vya udongo,kazi ya mikono ya mfinyanzi!

3 Hata mbwamwitu huwa na hisia za mamana kuwanyonyesha watoto wao;lakini watu wangu wamekuwa wakatili,hufanya kama mbuni nyikani.

4 Midomo ya watoto wachanga imekauka kwa kiu,watoto wanaomba chakula lakini hakuna anayewapa.

5 Watu waliojilisha vyakula vinonosasa wanakufa njaa barabarani.Waliolelewa na kuvikwa kifalmesasa wanafukua kwa mikono kwenye majaa.

6 Watu wangu wamepata adhabu kubwakuliko watu wa mji wa Sodomamji ambao uliteketezwa ghaflabila kuwa na muda wa kunyosha mkono.

7 Vijana wa Siyoni walikuwa safi kuliko theluji,walikuwa weupe kuliko maziwa.Miili yao ilikuwa myekundu kama matumbawe,uzuri wa viwiliwili vyao kama johari ya rangi ya samawati.

8 Sasa sura zao ni nyeusi kuliko makaa,wanapita barabarani bila kujulikana;ngozi yao imegandamana na mifupa yaoimekauka, imekuwa kama kuni.

9 Afadhali waliouawa kwa upangakuliko waliokufa kwa njaa,ambao walikufa polepolekwa kukosa chakula.

10 Kina mama ambao huwa na huruma kuuwaliwapika watoto wao wenyewe,wakawafanya kuwa chakula chaowakati watu wangu walipoangamizwa.

11 Mwenyezi-Mungu alionesha uzito wa ghadhabu yake,aliimimina hasira yake kali;aliwasha moto huko mjini Siyoniambao uliteketeza misingi yake.

12 Wafalme duniani hawakuaminiwala wakazi wowote wa ulimwenguni,kwamba mvamizi au aduiangeweza kuingia malango ya Yerusalemu.

13 Hayo yalisababishwa na dhambi za manabii wake,yalitukia kwa sababu ya uovu wa makuhani wakeambao walimwaga damu ya waadilifu mjini kwake.

14 Walitangatanga barabarani kama vipofu,walikuwa wamekuwa najisi kwa damu,hata asiwepo mtu yeyote wa kuwagusa.

15 Watu waliwapigia kelele wakisema:“Tokeni, nendeni zenu enyi mlio najisi!Tokeni, tokeni, msiguse chochote.”Hivyo wakawa wakimbizi na kutangatanga;watu wa mataifa walitamka:“Hawa hawatakaribishwa kukaa kwetu!”

16 Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwatawanya,wala hatawajali tena.Makuhani hawatapata tena heshima,wazee hawatapendelewa tena.

17 Tulichoka kukaa macho kungojea msaada;tulikesha na kungojea kwa hamutaifa ambalo halikuweza kutuokoa.

18 Watu walifuatilia hatua zetu,tukashindwa kupita katika barabara zetu.Siku zetu zikawa zimetimia;mwisho wetu ukawa umefika.

19 Waliotufuatia walikuwa wepesi kuliko tai,walitukimbiza milimani,walituvizia huko nyikani.

20 Walimnasa yule ambaye maisha yetu yalimtegemea,yule mfalme aliyewekwa wakfu wa Mwenyezi-Mungu,yule ambaye tulisema: “Chini ya ulinzi waketutaishi miongoni mwa mataifa.”

21 Wakazi wa Edomu, mwaweza kushangilia kwa sasa,mwaweza kwa sasa kufurahi enyi wakazi wa Uzi;lakini kikombe hiki cha adhabu kitawajia pia,nanyi pia mtakinywa na kulewa,hata mtayavua mavazi yenu!

22 Adhabu ya uovu wako ewe Siyoni imekamilika;Mwenyezi-Mungu hatawaacha zaidi uhamishoni.Lakini nyinyi Waedomu atawaadhibu kwa uovu wenu,atazifichua dhambi zenu.

Sura

1 2 3 4 5