27 Ni vema mtu kujifunza uvumilivutangu wakati wa ujana wake.
28 Heri kukaa peke na kimya,mazito yanapompata kutoka kwa Mungu.
29 Yampasa kuinama na kujinyenyekesha,huenda ikawa tumaini bado lipo.
30 Yampasa kumgeuzia shavu mwenye kumpiga,na kuwa tayari kupokea matusi yake.
31 Mwenyezi-Mungu hatatutupa milele.
32 Ingawa atufanya tuhuzunike,atakuwa na huruma tenakadiri ya wingi wa fadhili zake.
33 Yeye hapendelei kuwatesawala kuwahuzunisha wanadamu.