4 Siku hiyo watu watawasimanga kwa wimbo,watalia na kuomboleza kwa uchungu, wakisema:‘Tumeangamia kabisa;Mwenyezi-Mungu amechukua nchi yetu,naam, ameiondoa mikononi mwetu.Mashamba yetu amewagawia waliotuteka.’”
5 Kwa hiyo hamtagawiwa sehemu yoyote ya ardhimiongoni mwa watu wake Mwenyezi-Mungu.
6 “Usituhubirie sisi.Mambo kama hayo si ya kuhubiriwa.Sisi hatutakumbwa na maafa!
7 Je, yafaa kusema hivyo, wazawa wa Yakobo?Je, Mwenyezi-Mungu ameacha uvumilivu wake?Je, yeye hufanya mambo kama haya?”Sivyo! Maneno yangu huwafaa watendao mambo mema.
8 Lakini Mwenyezi-Mungu awaambia hivi:“Nyinyi mnawavamia watu wangu kama adui.Mnawanyang'anya mavazi yao watu watulivu;watu wanaopita kwenda zao bila wasiwasi,na wasio na fikira zozote za vita.
9 Mnawafukuza wake za watu wangukutoka nyumba zao nzuri;watoto wao mmewaondolea fahari yangu milele.
10 Inukeni mwende zenu!Hapa hamna tena pa kupumzika!Kwa utovu wenu wa uaminifumaangamizi makubwa yanawangojea!