7 Je, Mwenyezi-Mungu atapendezwanikimtolea maelfu ya kondoo madume,au mito elfu na elfu ya mafuta?Je, nimtolee mzaliwa wangu wa kwanzakwa ajili ya kosa langu,naam, mtoto wangukwa ajili ya dhambi yangu?
8 Mungu amekuonesha yaliyo mema, ewe mtu;anachotaka Mwenyezi-Mungu kwako ni hiki:Kutenda mambo ya haki,kupenda kuwa na huruma,na kuishi kwa unyenyekevu na Mungu wako.
9 Mwenyezi-Mungu anawaita wakazi wa mji,na ni jambo la busara sana kumcha yeye:“Sikilizeni, enyi watu wa Yuda;sikilizeni enyi mliokusanyika mjini.
10 “Je, nitavumilia maovuyaliyorundikwa nyumbani mwao,mali zilizopatikana kwa udanganyifu,na matumizi ya mizani danganyifu,jambo ambalo ni chukizo?
11 Je, naweza kusema hawana hatiawatu wanaotumia mizani ya danganyifuna mawe ya kupimia yasiyo halali?
12 Matajiri wa miji wamejaa dhuluma,wakazi wake husema uongo,kila wasemacho ni udanganyifu.
13 Kwa hiyo nami, nimeanza kuwaangusha chini,na kuwaangamiza kwa sababu ya dhambi zenu.