1 Maono ya Obadia. Mambo aliyosema Bwana Mwenyezi-Mungu kuhusu taifa la Edomu.Tumepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu;mjumbe ametumwa kati ya mataifa:“Inukeni! Twende tukapigane na Edomu!”
2 Mwenyezi-Mungu aliambia taifa la Edomu:“Nitakufanya mdogo miongoni mwa mataifa,utadharauliwa kabisa na wote.
3 Kiburi chako kimekudanganya:Kwa kuwa mji wako mkuu ni ngome ya miamba imarana makao yako yapo juu milimani,hivyo wajisemea,‘Nani awezaye kunishusha chini?’
4 Hata ukiruka juu kama tai,ukafanya makao yako kati ya nyota,mimi nitakushusha chini tu.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
5 “Kama wezi au wanyang'anyi wangekujia usiku,je, wasingechukua tu kiasi cha kuwatosha?Ikiwa wavunaji zabibu wangekujia,je, wasingekuachia kiasi kidogo tu?Lakini wewe, adui zako wamekuangamiza kabisa.
6 Enyi wazawa wa Esau, mali zenu zimetekwa;hazina zenu zote zimeporwa!