13 Msingeliingia katika mji wa watu wangu,siku walipokumbwa na maafa;msingelipora mali zao, siku hiyo ya maafa yao.
14 Msingelisimama kwenye njia pandana kuwakamata wakimbizi wao;wala msingeliwakabidhi kwa adui zaowale waliobaki hai.
15 “Siku inakaribia ambapo mimi Mwenyezi-Mungunitayahukumu mataifa yote.Kama mlivyowatendea wengine, ndivyo mtakavyotendewa,mtalipwa kulingana na matendo yenu.
16 Maana, kama walivyokunywa kikombe cha ghadhabu yangukwenye mlima wangu mtakatifundivyo na mataifa jirani yatakavyokunywa;watakunywa na kupepesuka,wataangamia kana kwamba hawakuwahi kuwapo duniani.
17 “Lakini mlimani Siyoni watakuwapo wale waliosalimikanao utakuwa mlima mtakatifu.Wazawa wa Yakobo wataimiliki tena nchi iliyokuwa yao.
18 Wazawa wa Yakobo watakuwa kama motona wazawa wa Yosefu kama miali ya moto.Watawaangamiza wazawa wa Esaukama vile moto uteketezavyo mabua makavu,asinusurike hata mmoja wao.Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.
19 Wale wanaokaa Negebu wataumiliki mlima Esau;wale wanaokaa Shefela wataimiliki nchi ya Wafilisti.Waisraeli watamiliki nchi za Efraimu na Samariana watu wa Benyamini wataimiliki nchi ya Gileadi.